KAMATI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MASHIRIKIANO KATI YA ZIAAT NA NBAA YAKUTANA LEO
POSTED ON: 21-07-2025
Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) ilitiliana saini hati ya mashirikiano ya utekelezaji wa majukumu mbali mbali baina ya Bodi hizo mbili tarehe 16 Mei, 2025 katika Ukumbi wa New Amaan Complex ulipofanyika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa ZIAAT
Kamati ya Utekelezaji wa Mkataba huo imekutana leo tarehe 21 Julai, 2025 yenye wataalamu kutoka ZIAAT na NBAA katika Ukumbi wa Mkutano wa ZIAAT
Pamoja na mambo mengine, Kamati hiyo itapitia utekelezaji wa Hati hiyo ya Mashirikiano ikiwa ni miongoni mwa ajenda kuu ya Mkutano huo