WANACHAMA WA ZIAAT WAPATIWA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO WA PSMIS

POSTED ON: 03-12-2025

Baadhi ya Wanachama wa ZIAAT leo tarehe 02 Disemba, 2025 wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa matumizi ya taarifa za wanachama (PSMIS). Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wanachama wote wa ZIAAT kutumia mfumo huo katika kujisajili kwa wale ambao hawajajisajili, kutengeneza nambari ya ankara (control no) kwa ajili ya malipo ya ada ya mwaka, kufuatilia mwenendo wa mafunzo yanayotolewa na ZIAAT pamoja na kuomba kufanya mitihani ya taaluma zinazotolewa na ZIAAT